ads

Rapa wa kike mkongwe kwenye muziki wa Bongo, Sister P, amesema kwa sasa hakuna msanii mwenye kasi iliyofikia enzi zao ama rapa wa kike mwenye uwezo mkubwa kama alivyokuwa yeye wakati anawika.

Akizungumza na Times FM ametoa mfano wa rapa Chemical akisema kunasehemu nyingine hajulikani kwa hiyo hasogei kwa kasi bali anajitahidi.

“Kasi tulikuwa nayo sisi enzi zile, sasa hivi hakuna anayekuja kwa kasi, huyu (Chemical) anajitahidi kiasi sio mchezo bado mapengo yetu yapo makubwa sana sasa hivi Fake wengi sana, umarekani mwingi mbwembwe mpaka wanaharibu.

“Siwezi kuwataja lakini nikisema fake kila mtu anajua, zamani ilikuwa game la muziki sasa hivi ni game la kibiashara” Alisema Sister P.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: