Dola za kimarekani Bilion 4 zinahitajika kuwekeza kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa ametoa
taarifa ya kiasi hicho cha fedha leo katika mkutano uliowakutanisha
wadau wa gesi nchini kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali
zitakazojitokeza baada ya kuupata mradi wa bomba la mafuta ghafi
linalotarajiwa kujengwa kutoka nchini Uganda mpaka Tanzania.
Prof. Ntalikwa amesema kuna fursa mbalimbali ambazo zitapatikana
sambamba na ajira kwa watanzania na ulipaji kodi ambao fedha zake
zitapelekwa kwenye huduma za jamii.
Amesema bado kuna mvutano wa bomba lijengwe Kenya au Tanzania na bado
wanaendelea na mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mvutano huo.
Prof. Ntalikwa amesema serikali itaendelea kuhakikisha miradi yake
inayoshirikisha nchi nyingine inasimamiwa kwa matarajio ya nchi.
Post A Comment: