Watu sita wamefariki dunia katika ajali iliyotokea katika Mlima Ipogolo baada ya Basi la Lupondije linalofanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza kupinduka baada ya mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema Dereva wa
basi hilo ambalo hufanya safari zake kati ya Iringa na Mwanza
alilazimisha kupita na abiria wote wakiwemo waliopaswa kushuka kituo
kikuu cha mabasi Iringa ili kuwahi moja ya mabasi yaendayo Mbeya kutokea
Dar es Salaam ili afaulishe abiria waliokuwa wanaelekea mkoani Mbeya.
Katika ajali hiyo jumla ya watu 38 wamejeruhiwa na baadhi yao
kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa ambapo 11 kati yao
wametibiwa na kuruhusiwa.
Post A Comment: