Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Alain-Aime Nyamitwe amesema
serikali yake inapanga kuipeleka Rwanda mahakamani kutokana na nchi hiyo
kuwaunga mkono waasi.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum aliyofanya na DW ambapo
waziri huyo amesema kila nchi ina haki ya kwenda mahakamani iwapo itaona
uhuru wake unakiukwa na kuongeza kuwa Burundi ina ushahidi unaoonyesha
kuwa Rwanda imekiuka uhuru na utu wa watu wa Burundi.
Wakati hayo yakijir Chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimemshutumu
Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa kile ilichodai kusababisha mauaji ya
kimbari nchini humo, wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili
unazidi kuzorota.
Mwenyekiti wa chama hicho, Pascal Nyabenda amesema katika taarifa
yake kwamba awali Rais Kagame alipanga jaribio la mauaji ya kimbari,
akimaanisha mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994 ambapo kiasi ya watu 800,000
waliuawa, wengi wao wakiwa Watusti.
Post A Comment: