Rapper wa muziki nchini Tanzania, Baghdad, ameamua kuandaa mixtape aliyo iita Old is Gold ambayo imekusanya nyimbo za zamani nakuzirudia tena studio ikiwemo Mtazamo ya Solo, Nikusaidiaje ya Profesa Jay na nyinginezo ambazo kwa mujibu wake Baghdad amesema tayari ameshapewa ruhusa ya kuendelea kuzifanya.
Lakini inasemekana kuna maneno ambayo Baghdad ameyazungumza yakasababisha mfarakano kati yake na Babu Tale kitu ambacho kime mpelekea Babu Tale amtoe kwenye kundi la Whatsapp kundi ambalo limekusanya baadhi ya wasanii wa Tanzania.
Kwenye remix ya Mtazamo aliyoimba Baghdad kunamistari ambayo ameimba "Game ishakuwa yawadau, Tale anaweza kukufanya media house ikuzarau, Kama hauna hela kajiunge Mkubwa Fela."
Akizungumza na mtembezi.com kuhusu suala hilo meneja huyo wa Tip Top Connection na Diamond Plutnumz Hamisi Tale, Babu Tale amesema kuwa hayupo tayari kumzungumzia rappa Bagh Dad.
Post A Comment: