Kamati ya bunge ya miundombinu imeelezea kuridhishwa na utekelezwaji
wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni jijini Dar es Salaam ambalo
limekamilika kwa asilimia 100 na litarajiwa kuzinduliwa aprili 15 na
kuanza kutumika aprili 16 mwaka huu.
Katibu mkuu wizara ya ujenzi Joseph Nyamhanga amewaambia wajumbe wa
kamati hiyo kwamba tayari mkandarasi amekwishalipwa asilimia 80 gharama
zote za ujenzi na kilichobaki ni kumalizia asilimia 20 iliyobaki.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Prof. RICHARD SIGALLA amesema kamati
imeridhishwa na mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2012 wakati
huo thamani ya dola moja ikiwa 1590 wasiwasi wa kamati ilikuwa ni
kuongezeka kwa gharama hizo kutokana na kupanda kwa dola jambo ambalo
serikali imeiondolea hofu kamati hiyo kuwa mpaka kufikia asilimia 80
thamani ya dola ni ile ile ya awali kwani hapakuwa na malimbikizo ya
malipo kwa mkandarasi.
Post A Comment: