Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Barcelona inakutana siku ya leo ili
kujadili namna ya kumuenzi gwiji wa kandanda Johan Cruyff aliyefariki
dunia wiki iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu.
Moja
ya jambo kubwa ambalo linasemekana litajadiliwa ni mabadiliko ya jina
la uwanja wa klabu hiyo Nou Camp ambao kuna mapendekezo upewe jina la
Cruyff ambaye aliwahi kushinda mataji ya La Liga na Copa del Rey kwenye
uwanja huo kabla hajatwaa mataji mengine mengi ya ulaya kwenye nyasi za
uwanja huo.
Rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu pamoja na viongozi wengine wanatarajiwa kukutana na familia ya shujaa huyo ili kufahamu namna zaidi ya kumuenzi.
Asilimia kubwa ya mashabiki wa Barcelona wametaka uwanja wa Nou Camp ubadilishwe jina na kupewa jina la mbabe huyo wa zamani wa soka ambapo asilimia 65 ya mashabiki wapatao elfu themanini waliopiga kura kwenye tovuti ya klabu hiyo wameridhia.
Wakati huo huo shirikisho la kandanda la Uholanzi KNVB limetangaza kuwa jina la uwanja wa taifa wa nchi hiyo Amsterdam Arena litabadilika na kuupa jina la Johan Cruyff ili kumuenzi mchezaji huyo.
Rais wa shirikisho hilo Michael van Praag amesema kuwa muda wowote jina hilo litabadilishwa.

Post A Comment: