Maambukizi ya UKIMWI yameanza kuongezeka tena kwa kasi mkoani Arusha
huku waathirika wakubwa wakiwa ni kundi la watoto wanaoishi katika
mazingira magumu,na wanaotoka katika familia maskini.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru Dk.Omary
Chande amesema hali hiyo inachangiwa na kuanza kupungua kwa kasi ya
kuhamasisha jamii kuepuka janga hilo kwa kuamini kuwa kwa sasa halipo
wakati bado lipo na madhara yake ni makubwa.
Mkurugenzi wa Shirika la World Education linalosaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu Kanda ya Kaskazini kupitia mradi wake
wa Pamoja Tuwalee Bi Lilian Badi amesema kasi ya upimaji wa UKIMWI
katika jamii imepungua kwa kiasi kikubwa na tatizo ni kubwa zaidi kwa
watoto wakiwemo wanaioshi katika mazingira magumu na wanaotoka katika
familia.
Akizungumza na watoa huduma za UKIMWI wa kujitolea zaidi ya 200
wanaopatiwa mafunzo ya kusaidia janga hilo yanayotolewa na Taasisi za
Pamoja Tuwalee na (CHSSC) zinazofadhiliwa na shirika la Misaada ya
Marekani (USAID) Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Ntabenda amewataka
watendaji kufufua upya kampeni za kukabiliana na UKIMWI.
Post A Comment: