Licha ya Serikali ya Marekani kupitia kupitia taasisi yake ya
Changamoto za Milenia(MCC), kuinyima Tanzania msaada wa fedha zaidi ya
tirioni 1 kutokana na matatizo ya kisiasa Zanzibar na sheria ya makosa
ya mtandao, Serikali ya Tanzania imesema imejipanga vizuri kuziba pengo
la fedha hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Waziri
wa mambo ya nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na kimataifa
Dr Agustine Mahiga, amedai japo uamuzi huo wa MCC umeiumiza serikali,
hawako tayari kuingiliwa katika mambo ya msingi ya nchi.
Balozi Mahiga alikiri kuwa uamuzi wa Bodi ya MCC utaathiri bajeti
ijayo ya serikali, kwa kuwa fedha hizo ambazo zingetolewa kwa kipindi
cha miaka mitano zingetumika katika miradi ya nishati ya umeme vijijini.
“Hivyo vyote Tanzania imekuwa ikisifika lakini kwa sababu hii
iliyotolewa na Bodi ya MCC kuwa Uchaguzi wa Zanzibar haukuwa huru na
haki na demokrasia haikufuatwa si za kweli, kwani Tanzania inazingatia
masuala hayo kwa mstakabali wa maendeleo ya Taifa.
“Uamuzi wa Washington tutaadhibiwa wote, Muha wa Kigoma na Mpemba wa
Pemba wote tutaumia. Huo ni uamuzi wao hatuwezi kuingilia, lakini na
yetu hatutaki yaingiliwe.
“Kwa suala la Zanzibar tumejitahidi kueleza pamoja na kuchukua hatua
ya kuimarisha demokrasia na tutaendelea kufanya hivyo,”alisema Balozi
Mahiga.
Post A Comment: