Meneja wa muziki wa Bongo flava, Hamis ‘Babu tale’ Tale, ametangaza
kuwa yupo tayari kusaidia kumpeleka ‘Rehab’ msanii yeyote atayemfata
kutaka kuacha madawa haramu ya kulevya.
Akizungumzia swala hilo, Babu Tale amedai anafanya haya akiwa kama mzazi, Mtanzania, mdau mkubwa wa Sanaa na Raia mwema.
“Mimi mzazi nina watoto wa kiume lolote linaweza kutoka, msanii
yeyote aliyekuwa tayari kuacha Unga aje nitampeleka Rehab kama
nilivyofanya kwa Chid Benz” Alisema.
Akizungumzia maendeleo ya rapper Chid Benz kwenye Rehab Bagamoyo,
amesema msanii huyo anaendelea vizuri na matibabu na anategemea kupata
ripoti kamili baada ya mwezi mmoja.
Post A Comment: