ads

Taasisi ya kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imewafikisha mahakamani wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tuhuma za rushwa.


Waliofikishwa mahakamani Kisutu Jijini Dar es salaam ni Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola CCM, Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa na Mbunge wa jimbo la Mvomero Sadick Murad.

Imeelezwa kuwa wabunge hao kwa pamoja wakiwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), waliomba rushwa ya shilingi milioni 30 kutoka katika halmashauri ya wilaya Gairo mkoani Morogoro ili kupitisha hesabu zake.

Wabunge hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti likiwemo la kulipa fedha taslim kiasi cha shilingi milioni 5 kila mmoja.

Katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na Spika wa Bunge Job Ndugai, wabunge hao walihamishwa kutoka katika kamati hiyo na kwenda kamati nyingine, ambapo Kangi Lugola aliyekuwa ndiye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo pamoja na Victor Mwambalaswa walihamishiwa katika kamati ya Mambo ya Nje huku Sadick Murad akihamishiwa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Wabunge hao watakuwa nje hadi April 15 kesi yao itakapotajwa tena.

Kufuatia tuhuma za kuwepo kwa rushwa katika kamati za Bunge kulipelekea wabunge wawili kujiuzulu katika kamati zao ambapo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe alijiuzulu ujumbe wa kamati akifuatiwa na Mbunge wa Nzega Mjini Hussen Bashe.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: