Aliyekua Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amelitaka
shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kufuata kanuni za CAF ilii
kufidia gharama walizoingia baada ya timu ya Chad kujitoa kushiriki
michuano ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) kutokana na
ukata.
Rage alisema kuwa tayari TFF imeingia hasara kubwa baada ya Chad
kujitoa dakika za majeruhi huku maandalizi ya mechi ya kimataifa yakiwa
yamekamilika kwa kiasi kikubwa hivyo amelitaka shirikisho hilo kufuata
kanuni za CAF ili kupata fidia ya gharama zilizotumika.
“Kwa kufuata kanuni za CAF za kujitoa mashindanoni ghafla lazima kuna
asilimia unazipata kutoka kwenye chama cha soka cha nchi husika ili
kufidia hasara hata kama sio asilimia mia moja.” alisema Rage.
Leo shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF litarudisha pesa za
kiingilio kwa washabiki waliokata tiketi kwa ajili ya kutazama mechi ya
Taifa Stars dhidi ya Chad baada ya wageni kujitoa dakika za majeruhi
huku gharama za kuweka timu kambini pamoja na maandalizi ya mchezo
zikiwa ndiyo zimepotea.
Rais wa TFF Jamal Malinzi alinukuliwa akisema hajawahi kufikiria
kutokea kwa tukio hilo na kutanabaisha bado hakuwa na jibu la moja kwa
moja la sakata hilo.
Kwa mujibu wa ratiba ya CAF Stars ilikuwa icheze mechi ya marudiano
jana March 28 dhidi ya Chad baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 mjini
N’Djamena Jumatano iliyopita.
Post A Comment: