Mahakama katika mji mkuu wa India imeamua kwamba ni kosa kwa mke
kumuita mumewe “ndovu” na kosa hilo linaweza kuwa msingi wa talaka.
Mahakama Kuu mjini Delhi imedumisha uamuzi wa mahakama ya chini uliotolewa mwaka 2012 ambao uliidhinisha talaka.
Mahakama hiyo ilisema mtu kumuita mumewe ndovu ni “kumtendea ukatili wa kiakili”.
Mfanyabiashara aliyeitwa ndovu ana umri wa miaka 35 na alikuwa na uzani wa kilo 100.
Alisema mkewe alizoea kumuaibisha kwa kuwa mnene na “kutoweza kutimiza haja yake ya kimapenzi”, vyombo vya habari India vimeripoti.
Mwanamke huyo alikuwa ameambia mahakama hiyo kwamba madai ya mumewe hayakuwa na msingi lakini mahakama haikukubaliana naye.
Post A Comment: