ads

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) amesema kitendo cha taasisi ya kupambana na rushwa hapa nchini TAKUKURU kuanza upelelezi juu ya kamati za bunge kukumbwa na kashfa za rushwa ni hatua nzuri ya manufaa na ya kuungwa mkono.


Zitto juzi alitangaza kujiuzulu katika Kamati Bunge Huduma za Jamii aliyokuwa akihudumu kwa madai ya baadhi ya wajumbe kupokea rushwa.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa 'Facebook' Mbunge Zitto amesema kwamba hatua inayochukuliwa na TAKUKURU ni hatua nzuri itakayopelekea ukweli kujulikana na watakaokutwa na makosa kuchukuliwa hatua stahiki.

''Uchunguzi wa vyombo vya dola ni moja ya njia muafaka ya kuhakikisha kila lisemwalo linakuwa na ukweli na pale ambapo suala limezushwa tu itajulikana na wazushaji hatimaye wataacha''-Amesema Zitto.

Aidha ikumbukwe kuwa baada ya tuhuma za rushwa katika kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mbunge Zitto Kabwe alimwandikia Spika wa Bunge Job Ndugai barua ya kujiuzulu akifuatiwa na Mbunge wa Nzega Mjini Hussen Bashe (CCM) ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo na ukweli uweze kufahamika.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: