ads

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa bila kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani basi hali ngumu za maisha za wananchi kwa wananchi wa chini haziwezi kubadilika kamwe. 


Sumaye aliyasema hayo jana akiwa katika uzinduzi wa kampeni za Udiwani katika Kata ya Kijichi jijini Dar es Salaam na kusema kuwa amezunguka nchi nzima na kuona jinsi watu ambavyo wanaishi katika mazingira magumu kutoka na hali ngumu ya maisha. 

"Tusipoipiga CCM chini Watanzania tutaendelea kuteseka, hali ya maisha itaendelea kuwa ngumu mtapigwa maneno ya hapa na pale lakini ukweli ni kwamba bila kuwaondoa hawa watu madarakani hali za maisha ya Watanzania hazitakuja kubadilika hata siku moja, tutaendelea kupondea mitumba, miguu ya kuku na utumbo, mtaendelea kukondeana, mtaendelea kupauka na ukiona mtu amenenepa ni kwashakoo tu si afya kwa sababu maisha ni magumu" alisema Sumaye 

Sumaye amedai ili Watanzania waepukane na maisha hayo ya hovyo ambayo sasa wanaishi wanapaswa kukipiga chini Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimeshindwa kuboresha maisha ya Watanzania toka nchi imepata uhuru mpaka leo. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: