ads

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema kiungo Jonas Mkude hastahili kucheza soka kwenye ligi ya Bongo kutokana na kiwango chake.


Rage ndiye kiongozi aliyemuuza aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mbwana Samatta kwenda Klabu ya TP Mazembe ambaye kwa sasa anaichezea Genk ya Ubelgiji.

Akizungumza na  gazeti la  Championi Jumatatu, Rage alisema kuwa, Mkude ni miongoni mwa wachezaji wazuri na hawastahili kuchezea katika klabu za hapa Bongo na badala yake anastahili kucheza katika timu za nje kama TP Mazembe na hata Ulaya, kikubwa ni kujitambua kwa mchezaji husika na kujituma ili aweze kufanikisha jambo hilo. “Mkude ni mchezaji mzuri, hakuna ubishi katika hilo na anayeamua kumchezesha ama kutomchezesha ni kocha.

“Nimpongeze kocha wa timu ya taifa, Salumu Mayanga kuweza kumrejesha tena katika kikosi cha timu ya taifa kwani ni mchezaji mwenye uwezo na walifanya makosa kumuacha katika kikosi hicho kwa kuwa ana uwezo. Nampenda kwa kweli.

“Ni mchezaji mwenye ‘future’ nzuri, lazima tukubaliane ana uwezo wa kucheza hata katika timu za nje kama TP Mazembe, Casablanca hata Ulaya, ninamtabiria atakuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye,” alisema Rage.

Credit - Champion
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: