ads

Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo nchini yameanza jana, Julai 31 jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

Imesema kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.

Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya nchi ipasavyo.

Williams imeelezwa ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo, akisema Barrick imepokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.

Rais aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine mbili, moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya kitaalamu iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga huo unaosafirishwa nje ya nchi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: