ads

Mshambuliaji  Barcelona, Neymar ameripotiwa kumshawishi kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho kuikatalia Barcelona ili wakaungane huko Paris Saint-Germain, taarifa zinadai.


Nyota hao wawili wa Kibrazili wamekuwa marafiki tangu walipokuwa na umri wa miaka minne na siku za karibuni Neymar alikuwa akimtaka Coutinho akajiunge na Barcelona kabla yeye kuripotiwa kwamba, anatakwenda PSG.

Wakati Liverpool wakiweka ngumu kumzuia Coutinho asiende Barcelona, imefichuka kwamba Neymar amekuwa akimtumia meseji za kupitia mtandao wa WhatsApp kumshawishi staa huyo wa Anfield asiende tena Nou Camp na badala yake amfuate rafiki yake huko Ufaransa.

Neymar amedaiwa kusafiri kwenda Qatar kukutana na bosi wa PSG kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake unaotajwa kwamba, utaweka rekodi mpya ya dunia kwenye usajili kutokana na wababe hao wa Ligi Kuu Ufaransa kuwa tayari kuvunja mkataba wa supastaa huyo kwa ada ya Pauni 196 milioni.

Baada ya kukamilika tu kwa mechi ya El Clasico huko Miami, ambapo Barcelona waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 huku Neymar akitegeneza mabao mawili kwenye mchezo huo, hakuungana na wenzake kurudu Barcelona na badala yake amekwenda Qatar kufanya mambo yake binafsi.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: