Wakazi zaidi ya 1,000 wa kijiji cha Mhande Kata ya Ng'ong'ona nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, hatimaye wameondokana na tatizo sugu la ukosefu wa huduma ya maji baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama zaid ya milioni 35.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima hicho, wananchi wamesema, tangu wahamie kijijini hapo miaka ya 1970 hawajawahi kupata huduma ya maji na wamekuwa wakichota maji umbali mrefu hali inayowalazimu kushindwa kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Mhande Jailos Hezron amesema, kijiji kimejipanga katika kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo ya maji iliyotengenezwa kwa gharama kubwa na serikali na kwamba mradi huo umekuwa mkombozi kijijini hapo
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme akizungumza na wananchi amesema, ujio wa mradi huo ni kutokana na ushirikiano kati ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mh. Anthony Mavunde, na wadau wa maendeleo kutoka nchini Canada ambapo amewataka wananchi kuutunza mradi huo ili kuondokana na adha ya ukosefu wa maji
Post A Comment: