Klabu ya Simba ambayo imepiga kambi katika mjini wa Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara 2017/2018 imepokea kipigo cha goli moja bila kutoka kwa timu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.
Mchezo wa jana wa Simba ambao umepigwa katika uwanja wa Orlando uliopo katika mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa klabu ya Simba katika maandalizi ya Simba Day
Baadhi ya mashabiki wa Simba wamepokea matokeo hayo kama changamoto katika kikosi chao huku wengi wakisema kuwa mchezo huo umesaidia kuimarisha kikosi chao na kuwafanya wachezaji kuwa pamoja.
Klabu ya Simba ni moja ya kati ya timu ambazo msimu huu zimesajili wachezaji wengi ikiwa ni lengo la kuimarisha kikosi hicho kuelekea katika msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2017/2018.
Post A Comment: