ads

Waziri Kivuli wa Mipango, Fedha na Uchumi, Halima Mdee ameitaka Serikali kujibu hoja kuhusu kuporomoka kwa uchumi katika utawala wa Rais John Magufuli badala ya kuwadanganya wananchi.


Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema) amesema hoja zilizotolewa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazijajibiwa na Msemaji wa Serikali, Dk Hussein Abbas badala yake anatoa takwimu za uongo.

Amebainisha hoja mbalimbali zinazohitaji majibu kuwa ni Serikali kueleza kwanini kilimo kimeporomoka na itoe mpango mkakati wa kuinua kilimo nchini.

Pia, amehoji kushuka kwa uchumi wa benki ambazo hazitoi mikopo kwa wafanyabiashara.

"Tulichokuwa tunakizungumza juzi ndiyo hicho wamekizungumza jana watu wa TPSF. Serikali imeondoa fedha zake kwenye benki za biashara na kwenda kuzifungia BOT. Huku kwenye mzunguko hakuna hela," amesema.

Hata hivyo, Mdee amesema katika bajeti ya mwaka 2017/18, Serikali inatarajia kukopa Sh7 trilioni, mkopo wa ndani ukiwa ni Sh6 trilioni na mkopo wa nje Sh1 trilioni.

"Serikali hii ambayo haizisaidii benki zake zichanue, ndiyo hiyo hiyo inategemea kukopa Sh6 trilioni kwenye benki hizo hizo," amesema Mdee.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: