Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ameridhia utenguzi wa wabunge nane wa CUF waliofukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi CUF ambalo lipo chini ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa Profesa Lipumba.
Spika wa Bunge ametangaza kuwa nafasi hizo nane hivi sasa ziko wazi
Wabunge hao nane wa viti Maalum wa CUF ambao wamefukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), awali kabla ya maamuzi haya ya spika wa Bunge walisema kwamba watakwenda mahakamani kutafuta haki yao kwa kuwa wao hawamtambui Lipumba na Baraza lake na kusema uongozi huo ulitoa taarifa hizo ni batili.
Post A Comment: