Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene amesema polisi wamemchukua Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu na kwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari leo Ijumaa, Julai 22, Makene amesema mpaka sasa haijajulikana upekuzi huo unahusu kitu gani.
“Polisi hadi sasa hawajafafanua tuhuma za uchochezi ambazo Tundu anakabiliwa nazo, iwapo zinahusu uchochezi wa akina nani, kwa ajili ya nini,” imesema taarifa hiyo.
Kadhalika, Wakili wa Lissu, Fatma Karume alithibitisha Lissu kupelekwa nyumbani kwake na polisi hao.
Post A Comment: