Baada ya kulazwa hospitali kwa muda wa siku tatu , muigizaji wa filamu za vichekesho Mzee Majuto ameruhusiwa na kurudi nyumbani kwake baada ya kufanyiwa upasuaji wa hernia (ngiri) mkoani Tanga.
Akizungumza kwa njia ya simu mke wa Mzee Majuto Bi. Aisha Majuto amesema kwamba tatizo lililokuwa likimsumbua mumewe lilianza siku nyingi ingawa kwa wiki iliyopita hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi hadi kufikia kulazwa.
"Ni kweli tulikuwa tumelazwa lakini mume wangu amesharuhusiwa na kurudi nyumbani. Tatizo ni hernia (ngiri) na ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri ingawa hawezi kuzungumza kwa muda mrefu", Bi Aisha Majuto.
Post A Comment: