ads

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia muuguzi wa kituo cha afya cha kata ya Igulubi, Damiana Mgaya (26) kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 18, baada ya kumchoma sindano ya usingizi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa, alisema muuguzi huyo ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani upepelezi utakapokamilika.

Alisema msichana huyo (jina limehifadhiwa), alipatiwa fomu ya PF3 baada ya tukio hilo na jana aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya hali yake kuendelea vizuri.

“Hali ya huyu msichana imeimarika na ameruhusiwa, naye atahojiwa kwa upande wake ili tujue uhalisia wa tukio lilivyokuwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Kamanda huyo alisema siku ya tukio msichana huyo alifika kwenye Zahanati hiyo kwa ajili ya kumuuguza mama yake mzazi, ndipo muuguzi huyo alipotumia nafasi hiyo kumchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka.

Akizungumza na Nipashe juzi, Mtendaji wa kata ya Igulubi, Ntemi James alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa 8 usiku hadi alfajiri, wakati msichana huyo akimuuguza mama yake aliyelazwa katika kituo hicho.

Ntemi alisema mtuhumiwa Damian alimpokea mama wa msichana huyo akiwa hoi na kumlaza kwa matibabu.

Alisema kuwa muuguzi huyo alimchoma sindano ya usingizi mama yake na kisha alimfuata msichana huyo na kumwambia waende chumba kingine kwa ajili ya kuchukua dawa.

Alidai kuwa alipofika kwenye chumba hicho, mtuhumiwa alimwambia msichana huyo kuwa inabidi amchome sindano ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali siyo masafi.

Aliendelea kusimulia kuwa msichana huyo alikubali kuchomwa sindano mbili zilizomsababishia kuishiwa nguvu hadi alipozinduka asubuhi.

Ntemi alisema asubuhi mama mtu alimwamsha mwanaye akiwa hajitambui na kugundua kuwa sehemu zake za siri zilikuwa zimeingiliwa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete, alithibitisha kubakwa kwa msichana huyo baada ya kupata taarifa kutoka timu ya wataalamu aliyoituma kutoka wilayani.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: