ads

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amesema kwa beki waliyonayo sasa hivi kikosini mwao, ni wazi watani wao Yanga wataisoma namba hasa baada ya kusajiliwa Salim Mbonde kutoka Mtibwa Sugar.


Simba imemsajili Mbonde kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo kuongeza idadi ya mabeki wakiwemo Shomari Kapombe aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Ally Shomari (Mtibwa) na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ aliyepo kikosini.

Simba inaweza kuwajaribu mabeki hao Agosti 23, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es

Salaam. Akizungumza na gazeti la  Championi , Mkude amesema ujio wa Mbonde katika kikosi chao umeleta chachu kwa kuwa na mabeki imara ambao wanaifanya timu kubwa bora kupambana na timu yoyote hata Yanga.

“Ujio wa Mbonde Simba umeongeza ushindani katika safu yetu ya ulinzi pia inakifanya kikosi chetu kiweze kuwa imara zaidi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, Yanga wajiandae.

“Tutakutana nao kwanza katika mechi ya Ngao ya Jamii, tupo vizuri na kwa safu yetu hii ya ulinzi naamini Yanga watapata tabu kutupita tofauti na huko nyuma,” alisema Mkude.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: