ads

Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek ni mwanaisimu na mwandishi Mjerumani aliyeishi nchini Afrika Kusini. Anajulikana hasa kwa kuandika kitabu cha sarufi ya Kizulu pamoja na tafiti nyingi za lugha za Kibantu. Neno Bantu, maana yake ni watu


Bleek aliyeishi tangu mwaka mwaka 1827 hadi 1875  ndiye aliye linganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu na kuziunganisha, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.

Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo.

Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Swaziland na Afrika ya Kusini.

Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: