ads

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu ameshikiliwa kwa muda polisi baada ya kutokea vurugu katika kikao cha kamati ya siasa ya chama hicho.


Dk Nagu aliyewahi kuwa waziri katika wizara kadhaa wakati wa utawala wa Serikali za awamu mbili zilizopita, alishikiliwa kwa muda jana, Julai 18 na kuachiwa baada ya kuhojiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Masawe amesema Dk Nagu alifikishwa kituoni kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye kikao cha kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Hanang baada ya makundi mawili kujitokeza.

Masawe amesema baada ya mahojiano kufanyika na kuandika maelezo, kwa kuwa mgogoro huo ulikuwa ni mambo ya ndani ya CCM walimwachia.

"Taarifa ambazo nimepata ameachiwa baada ya kuandika maelezo na tayari walifikia makubaliano wenyewe," amesema.

Awali, mkuu wa wilaya hiyo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, Sara Msafiri amesema: "Ni kweli amekamatwa lakini nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza.”

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zimeeleza Dk Nagu alikamatwa kutokana na malumbano ya kupitisha wagombea wa uchaguzi ndani ya CCM.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: