ads

Ndugu zangu Watanzania,

Nimesoma kwa umakini "Taarifa" ya kukamatwa na kupelekwa Kituoni Katibu Mkuu wa Chadema na Viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Kanda, kule Mbamba Bay, wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Mara kadhaa viongozi wa vyama mbali mbali pia wamekamatwa. Nimeshindwa kuelewa hasa tatizo la Msingi ni nini kwa kuwa Taarifa zinatolewa kwenye mitandao ya Jamii ki ushabiki zaidi. 


Hivyo mtu yeyote makini mwenye nia ya kulisaidia Taifa au kwa kushauri au kukemea anashindwa kwa kuwa " facts za msingi" haziwekwi wala kujadiliwa; wala na mtoa " thread/post au hata na wachangiaji. Namshukuru Mkurugenzi Kibatala, Wakili Msomi Mallya na wasaidizi wake mara kadhaa wamejaribu kutoa ufafanuzi katika hatua ya kesi lakini bila facts za matukio. Ni wazi katika hatua hiyo siyo jukumu lao kutoa facts kwa kuwa itaharibu kesi yao.

Hata hivyo, baada ya kusoma mara kadhaa Taarifa ya matukio haya nimepaswa kurejea Political Parties Act, ( RE 2002) na Kanuni zake zote.

1) Kimsingi, Watu wengi wanaamini kuwa Vyama vya siasa viko huru kufanya Mikutano ya ndani bila kutoa " Taarifa" ( Notice) Taarifa kwa Mamlaka husika ya Police katika eneo. Kifungu cha 11 (1-7) chahusika. Hii ni imani iliyojengwa visivyo, na utaratibu huu usipofuatwa wahusika hulalamika kuwa wanakandamizwa na kunyimwa haki za kidemokrasia na yote yanayoendana na hayo.

Ili sisi tusioegemea upande wa Chama chochote, bali ni Wapenzi wa Taifa na kwa Taifa lolote katika ulimwengu wa leo vyama imara ni muhimu kwa maendeleo ya Kiuchumi na kisiasa. Ninaomba mwenye facts za matukio haya atuwekee ili tuweze kujadili with " objective and unbiased observations". Ebu tuachane na kauli zisizojengwa katika misingi ya kisheria kuwa " mikutano ya ndani haihitaji utoaji wa Taarifa". Ni kweli Mikutano ya Vyama vya siasa iwe ya nje au ya ndani haihitaji " Kibali cha yeyote wakiwemo Polisi ( Hukumu ya Mahakama Kuu).

2. Pamoja na maelezo hayo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa niliyotaja hapo Juu, mamlaka ya Polisi katika kudhibiti vyama vya siasa yapo pale pale iwapo utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na utaratibu uliowekwa na Sheria na Kanuni haukufuatwa. Utaratibu huo ni pamoja na kutoa " Notice" ( Taarifa) kwa Mamlaka husika ya Polisi katika eneo husika.

a) Iwapo utaratibu wa kutoa Taarifa umefuatwa, Mamlaka ya Polisi hayawezi kukataza mkutano ulioombwa ( wa ndani au wa nje) isipokuwa kwa sababu zilizotajwa ndani ya Sheria.

b) Taarifa za Ki-inteligensia au kugongana mikutano ya vyama ni sababu mojawapo ya mamlaka husika kuzuia mkutano uliotolewa Taarifa. Lakini Mamlaka hiyo inatakiwa kutoa siku/ muda mwingine au hata eneo lingine/ uwanja mwingine Mkutano huo unapotakiwa kufanyika. Hili ni hitaji la kisheria na siyo hisani ya mtu au kiongozi yeyote,

3) Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vya Siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisasa, ya ndani na ya hadhara kwa lengo la kutafuta wanachama. Haina mantiki kuwa na "ndoa" ambayo wana ndoa hao wanawekewa masharti wasipate watoto kwa utaratibu ulioko ndani ya masharti ya Taratibu zilizoko katika Imani iliyowaunganisha katika ndoa hiyo. Kufanya hivyo ni kumaliza kizazi cha wana ndoa hao. Mimi siamini na sijaona mahali popote "Decree" ( Amri ya Rais) inayozuia Mikutano ya vyama ya nje wala ya ndani. Aliyeiona aniwekee humu jukwaani, Hivyo siamini kabisa kama kuna Katazo la Rais, ukiacha matamko ya kisiasa. Kauli ya Rais si sheria na haiwezi kuvunja Sheria iliyotungwa na Bunge ( Sheria na 5 ( RE 2002 ni sheria halali iliyotungwa na Bunge). Ninaamini kabisa kama kuna amri yeyote ya Rais, chama makini kingeli " challenge" amri hiyo chini ya vipengele vya sheria vya " Prerogative Orders za Certiorari, Prohibimus na Mandamus". Wanasheria wanajua vizuri matumizi ya sheria hizo katika kudhibiti matumizi mabovu ya mamlaka ya kuiongozi yeyote. Hivyo, tusitafute majibu mepesi katika " udikteta". Ni muda mwafaka sasa kutafuta majibu sahihi penginepo.

4) Ni wazi kabisa, na nimemsikia Waziri wa Mambo ya ndani akitamka mara kadhaa kuwa mikutano ya Vyama ( ya hadhara na ya ndani ) haijapigwa marufuku alimradi utaratibu unafuatwa. Ni kwa msingi huu, ningependa sasa wapenzi wa vyama kuanza kubana viongozi wao kujua kama kweli " Taratibu" zote zilizowekwa na sheria zimefuatwa katika maandalizi ya mikutano ya vyama vya siasa. Tukumbuke Sheria yetu ya Vyama vya Siasa ni ya 1992 ( RE -as amended 2002) na Kanuni zake na tukumbuke Sheria inayoongoza Jeshi la Polisi ni za 1959 ( kama sikosei- sijacheki- na marekebisho madogo madogo kadhaa yakiwemo ya 2002). Hivyo Rais aliyeko madarakani kwa kutambua uwepo wa sheria hizo na kuzisimamia kama alivyoapa kusimamia Katiba na sheria hawezi kulaumiwa. Tangu ameingia madarakani siku takriban 600 zilizopita Rais aliyepo chini yake hapajatungwa sheria yeyote ya kudhibiti vyama na wala hakuna marekebisho yaliyofanyika, labda kama yamenipita pembeni, basi nielimishwe.. Katika hali hiyo tusipende kutafuta majibu mepesi kishabiki bila kufanya utafiti wa kina wa Tatizo linalosibu Taifa na Demokrasia yetu.

5) Ni kweli Pia kuwa Polisi kwa kutumia Sheria za zamani zisizoendana na wakati, na bila waendesha Kesi wa Serikali ( kama ilivyo desturi katika kesi nyingi) kufanya maandalizi mazuri kesi nyingi zinazofunguliwa chini ya kinachoitwa kesi za " uchochezi" ( ambazo mimi mwenyewe kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama nilifunguliwa) au hasiendelei, au hatimaye hushindwa mahakamani kwa kukosa maandalizi hafifu ya Prosecutors au kwa kesi zenyewe au ukamataji kukosa misingi ya kijinai katika mazingira halisi ya leo. Ni wazi kesi hizi huchafua siyo tu jina la Serikali iliyoko madarakani bali pia sifa nzuri ya Taifa letu. Ni muhimu Maofisa Polisi kutimiza majukumu yao kwa umakini mkubwa na uangalifu mkubwa, na hasa kufuata misingi ya kisheria na kulinda Sheria za nchi bila kufanya mambo kwa kumpendeza mtu yeyote awaye. Taifa ni letu sote, mambo yakiharibika, sote tutaumia pamoja na mamlaka zenyewe za polisi, kwani leo uko kwenye madaraka kesho atakuwepo mwingine.

6) Maelezo kuwa Chama Tawala kinafanya "Mikutano" ( ya ndani au ya nje) haiwezi kuwa hoja yenye nguvu. Kwani kama " wametimiza hitaji la " Notice" inayohitajika kisheria kama utaratibu wa kisheria unavyotaka lazima wapige "mbiu" au wawatangazie. Nani kafanya utafiti kwenye ma faili ya mamlaka husika kuwa "hawakufuata" utaratibu wa kisheria. Hii ni hoja dhaifu sana kuhalalisha "kutotafakari na kufanya utafiti" katika wa kina.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa, inauma kila siku kuona viongozi wa vyama wakikamatwa, na baada ya muda kuachiwa mahakamani. Ni dhahiri kuna dosari mahali. Au waliokamata hawakuwa makini, au walikuwa wakitaka kumpendeza au wanajipendekeza kwa malengo wanayojua wenyewe. Au kama nilivyoeleza Waendesha Mashtaka wa Serikali, DPP na wasaidizi wake wakiwemo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajiandai vizuri.

Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama. Viongozi wawe wazi kama wamefuata Taratibu za kisheria au wamezoea kufanya mambo kwa " mazoea tu". Hakuna mahali popote sheria inapotamka kuwa "Mikutano ya ndani ya Vyama" haihitaji " Notice". Wala Mamlaka ya Polisi hasa vifungu vya 43, 44 etc vya Police Ordinance, ( kama sijakosea) havijarekebishwa wala kuondolewa, hivyo vikitumika tusilalamike, bali tuwalalamikie viongozi wetu kwa kutokuwa " Proactive" vifungu hivyo vilivyotungwa wakati wa ukoloni vifanyiwe marekebisho ya msingi ili demokrasia ya kweli iweze kujenga msingi katika Taifa letu. Wanasheria wa vyama ningelipenda wawasaidie wapenzi wa vyama katika kutoa elimu ya msingi, lakini pia kuwashauri vizuri pia viongozi badala ya kusubiri " kesi mahakamani".

Nawasilisha.

Credit - Jamii Forum
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: