Kipa Aishi Manula amesema wakati ukifika, ataeleza anakwenda timu ipi.
Manula amesema angependa suala la amekwenda timu ipi apewe muda.
“Muda ukifika nitaeleza, naomba mvute subira,” alisema kipa huyo namba moja wa Taifa Stars baada ya kurejea nchini akitokea Rwanda.
Hata hivyo, tayari Manula ameishasaini Simba mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC.
Lakini suala la anakwenda Simba limeendelea kuwa siri kwa kuwa mkataba wake haujaisha na Azam FC.
Post A Comment: