Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekataa ombi la Mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth la kumruhusu mteja wao kwenda nje ya nchi kutibiwa uvimbe uliopo tumboni na badala yake apatiwe tiba kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mawakili hao wametoa ombi hilo mblele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwa kusema mteja wao anasumbuliwa na uvimbe na Baloon tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa wiki ya nne sasa
Mfanyabiashara Harbinder Singh pamoja na James Rugemalira walipandishwa mahakamani leo Julai 14, hata hivyo wakili wa serikali, Leornad Swai ameileza mahakama kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Julai 22.
Harbinder Singh Sethi mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, pamoja na mfanyabiashara James Rugemalira wanakabiliwa na mashtaka yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.
Post A Comment: