ads

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.


Hayo yamewekwa wazi na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake ACP Barnabus D. Mwakalukwa .

Mabadiliko hayo, yanamgusa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda sasa amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne ambaye alikuwa Kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Mabadiliko mengine soma hapa 

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: