ads

Chama chetu cha Act Wazalendo ni kichanga Kwa umri lakini ni kibobevu kwenye Uongozi. Unajua uimara wa Vyama kwenye mitihani Kama Hii inayotukuta sisi. Tunavuka na Mola anatusaidia kuishinda mitihani. 


Kuna ambao toka tuanzishe Chama wameshindwa kukubali hali halisi na ku move on. Kila siku wanatushambulia Kwa kejeli na maneno. Sisi hatuwajibu. Tunafanya yetu. Hatuwashangai maana tunawaongoza kwenye hoja. Tutaendelea kuwaongoza kwenye hoja. Hatubabaishwi na kelele zao. 

Hakuna Chama Cha Siasa nchi Hii kinaweza kuthubutu kubeza uwezo wetu wa hoja na kuchambua hoja. Kelele hatuna. Matusi hatuna. Kebehi hatuna. Hoja hapa ni mtakuja. 

Wanachama 400,032 wa ACT Wazalendo mliotapakaa nchini nzima msiingie kwenye malumbano na nyumbu. Nyumbu hawawazi. Wanafuata tu. Wajibu wetu ni kuwaongoza nyumbu wavuke salama mto mara. Asili ya kuanzishwa kwetu ni kuukataa unyumbu. Tuendelee kuukataa unyumbu Kwa kumrejea Nkrumah " Forward Ever, Backward Never ". 

Sisi ni Gogo la Udi. Unavyolichoma ndio linavyonukia. 

Utu. Uzalendo. Uwajibikaji.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: