Yanga imemalizana na mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba.
Ajibu amejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.
Taarifa kutoka Yanga zinaeleza Ajibu amemalizana na Yanga mchana huu baada ya kuwa wamefanya mazungumzo mfululizo tokea juzi.
"Tulikuwa hatujamalizana katika masuala fulani ya fedha, lakini sasa naona mambo yamekaa vizuri kabisa," kilieleza chanzo.
"Ukisema Ajibu ni mchezaji wa Yanga tayari, wala hautakosea," chanzo kilisisitiza.
Post A Comment: