ads

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameonyesha kushangazwa na bajeti iliyowasilishwa bungeni leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.


“Kwa kweli hii haijawahi kutokea, ni kwa miaka mingi hatujawahi kuona bajeti nzuri kama hii.” amesema Ndugai.

 Ndugai ameyasema hayo leo (Alhamisi) mara baada ya Waziri Mpango kuhitimisha kuwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18 huku asilimia kubwa ya wabunge wakimpigia makofi Waziri huyo.

Ndugai ameisifia bajeti hiyo akisema kwa miaka mingi ya uwasilishwaji wa bajeti za Serikali bungeni haijawahi kutokea wabunge wakaipokea vizuri kiasi hicho.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: