Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.
Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.
Pamoja na hayo, Waziri Mpango ameshuha ushuru kwa mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu zinazozalishwa ndani kutoka Sh2O2 kwa lita hadi Sh200 kwa lita.
Kadhalika ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Sh429 hadi 450 kwa lita.
Wakati huo, ushuru wa bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka Sh534 hadi Sh564 kwa lita.
Post A Comment: