Wakala Mino Raiola anayemsimamia Mario Balotelli, amesema nafasi kubwa ya mchezaji huyo ni kutua Borussia Dortmund msimu ujao.
Sababu za klabu hiyo ya Dortmund kuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa timu ya Nice, ni kutokana na kuwapo taarifa za msambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang kuhitajika Paris Saint-Germain.
Riola alifanya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo jana Jumanne, huku akisema ana uhakika mchezaji huyo atakipiga Dortmund msimu ujao.
Post A Comment: