Mke wa Waziri Mkuu mteule wa Lesotho, Lipolelo Thabane ameuawa kwa kupigwa risasi ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuapishwa kwa mume wake, Thomas Thabane.
Lipolelo ameuawa jana (Jumatano) wakati akiendesha gari karibu na nyumbani kwake, katika mji mkuu wa Maseru.
Taarifa zinaeleza kuwa Thabane ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, alitengana na mwanamke huyo tangu 2012.
Historia inaonyesha kuwa mwaka 2014 wanajeshi walijaribu kumpindua Thabane kutoka madarakani.
Uchaguzi uliofanyika nchini Lesotho mapema mwezi huu ni wa tatu katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na migogoroy kisiasa.
Waziri Mkuu huyo ataapishwa Ijumaa.
Post A Comment: