Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa uamuzi wa kumvua uenyekiti uliochukuliwa na chama chake cha ACT-Wazalendo, umefanyika mapema.
Mghwira ameyasema hayo leo Alhamisi katika Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro mjini hapa, mara baada ya kutia saini kitabu cha wageni.
Hata hivyo, RC huyo mpya amesema hatua hiyo itampunguzia mzigo na kumrahisishia kazi tofauti na angeendelea kutumikia uenyeketi wa chama huku akiwa mkuu wa mkoa kwa wakati mmoja.
Mghwira ambaye alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na mgombea wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia chama hicho, aliteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
"Mimi siyo mpinzani wa maendeleo nimepewa jukumu la kutekeleza maendeleo ya nchi," amesema Mghawira.
Mghwira ameongeza kuwa kwa nafasi aliyopewa atafanya kazi kwa kufuata Ilani ya CCM aliyopewa na Rais John Magufuli.
Post A Comment: