Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amemsifu marehemu Abdul Mtiro kuwa alikuwa hodari, mchapakazi na mtiifu.
Mtiro maarufu Cisco amewahi kuwa Mkuu wa Itifaki katika Serikali za awamu ya nne na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.
Mtiro aliyefariki dunia Jumatatu, alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Membe aliyekuwa pamoja na viongozi wengine wakiwamo marais wa awamu ya pili na ya nne, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete alisema umati huo wa watu unaonyesha tafsiri ya utumishi uliotukuka wa kiongozi huyo.
Membe aliwahi kuwa bosi wa Mtiro wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
“Balozi Cisco alikuwa anaijua dunia kama anavyoijua Tanzania, Tunamkumbuka kwa uhodari katika kazi na utiifu,” alisema.
Alisema marehemu Mtiro alikuwa mwalimu mzuri kwa maofisa wa mambo ya nje hasa kwenye masuala ya itifaki.
Post A Comment: