ads

Mohamed Salah amempokonya jezi Roberto Firmino huko Liverpool, lakini hiyo tisa, 10 ni jinsi kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp kitakavyokuwa msimu ujao, nakwambia wapinzani wajipange.


Awali, iliaminika kwamba staa huyo ghali kabisa Anfield angekubali kuiacha jezi Namba 11 na kuchukua Namba 9 kwa kuwa ilikuwa ikivaliwa na Firmino, lakini badala yake amechukua Namba 11 aliyokuwa akiivaa huko AS Roma na Mbrazili Firmino sasa amechukua Namba 9.

Lakini, ujio wa Salah katika kikosi hicho kinaifanya Liverpool kuwa na moto mkali kweli kweli kwa msimu ujao.

Cheki tu, Sadio Mane atakuwa anakimbiza kutokea upande wa kushoto na Salah, ambaye anadaiwa mshahara wake wa wiki utakuwa Pauni 90,000 kwa wiki atakuwa anakimbikiza upande wa kulia.

Ujio wa staa huyo wa Misri unamfanya Klopp sasa kuwa na kikosi matata kabisa kinachoendana na fomesheni yake ile ya 4-3-3, ambapo kwenye safu ile ya ushambuliaji itakuwa na watu watatu matata, Mane, Salah na Firmino, wote wanakimbiza, huku kwenye safu yake ya kiungo kutakuwa na Philippe Coutinho, Adam Lallana na Jordan Henderson.

Kwenye ule ukuta wake wa mabeki wanne utakuwa na vichwa matata tupu, Nathaniel Clyne atakuwa upande wa kulia, kushoto ni James Milner na mabeki wa kati ni Dejan Lovren na Joel Matip, wakati kwenye goli atakuwa Simon Mignolet.

Kwa kikosi hicho cha Klopp, hapo kwenye benchi atakuwa na kiungo Georginio Wijnaldum, Emre Can na kwenye straika kutakuwa na Divock Origi, Daniel Sturridge na Danny Ings. Ni hatari!
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: