Chama cha ACT-Wazalendo kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kikieleza kuwa amevunja mwiko wa siasa za Tanzania baada ya kufanya teuzi kutoka katika vyama pinzani ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Samsoni Mwigamba wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kwa hatua hiyo aliyoonyesha Rais Magufuli, sasa ni wakati wa watanzania kuanza kuona kuwa taifa hili ni letu sote.
Aidha, Mwigamba amesema kuwa chama chao hakioni tatizo lolote kwa uteuzi wa aliyekuwa mwenyekiti wao, Anna Mghwira ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, huku akisisitiza kuwa ni jambo jema kwani ameteuliwa ili akawaatumikie wananchi. Tazama hapa
Post A Comment: