Rais John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 15 Aprili, 2017.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, inaeleza kuwa Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota.
Mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajiwa kuwa na idadi ya nyumba 644 za makazi.
Post A Comment: