Kijana wa miaka kumi na tatu huko Marekani, amepoteza maisha baada ya kujipiga risasi bahati mbaya huku marafiki zake wakimuangalia kupitia Instagram Live.
Mama yake, Shaniqua Stephens amesema alisikia kishindo kikubwa kwenye chumba cha mwanae, Malachi Hemphill, 13. Yeye na mtoto wake wa kike walikimbia ghorofani na kumkuta mwanae akiwa amelala kwenye dimbwi la damu. Simu yake ilikuwa ikionesha Instagram Live.
Mtoto huyo alikuwa live Instagram akichezea bunduki kuwaonesha followers wake. Alikimbizwa hospitali ambako alipoteza maisha.
Polisi wanapeleleza kubaini ni kwa vipi Malachi alipata bunduki.
Post A Comment: