Mabweni mapya ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yana uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 3,840 kwa uwiano wa wanafunzi 192 kwa kila jengo.
Akizungumza leo wakati Rais John Magufuli akizindua mabweni hayo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, mabweni hayo ni mjumuiko wa majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja na vyumba 12 kwa kila ghorofa.
Profesa Mukandala amemwambia Rais Magufuli kuwa chuo chake kimechangia ujenzi wa mabweni hayo kwa kutengeneza vitanda 1920, makabati 1920, droo 1920, meza 1920, viti 3,840 na magodoro 3,840.
Post A Comment: