Baada ya tetesi kuzagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Jux ameachana na mpenzi wake Vanessa Mdee, Jux ameshindwa kufunguka hukusu sakata hilo.
Muimbaji huyo amedai yupo kwenye mahusiano huku akishindwa kueleza anaendelea kutoka na Vanessa au amepata mrembo mwingine.
Akiongea katika kipindi cha FNL cha EATV, Jux amedai yeye naendelea na shughuli zake za muziki na Vanessa yupo nje ya nchi kwaajili ya shughuli zake za muziki.
“Kwanza nataka kukusahihisha kuwa mimi sio single boy, niko na mtu,” alisema JUX. “kuhusu Vanessa kama nipo naye that my business,”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya wimbo wake mpya.
Post A Comment: