ads

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta   kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.


Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliifuta kesi hiyo leo chini ya kifungu cha 225 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya  jinai (CPA).

Kesi hiyo imefutwa baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Maugo kueleza kuwa hawakuwa na shaidi na kuomba wapewe ahirisho.

Katika uendeshwaji wa kesi hiyo upande wa mashtaka uliita ushahidi mmoja kwa miezi 14.

Katika kesi hii, Gwajima anadaiwa kuwa  kati ya Machi 16 na 25,2015 Tanganyika Packers Kawe alitumia lugha chafu na kumdhihaki  Muhadhama wa Kanisa Katoliki  Askofu Kardinal Polcarp Pengo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: