TAFITI za kisayansi zilizofanywa hivi karibuni zimebaini kuwa, nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.
Utafiti huo umeofanywa katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zinazotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.
Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama vile jijini Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga mimbao katika nyumba ya uzazi ya mwanamke
Akizungumzia utafiti huo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, amesema kuwa, upo ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.
Amesema kuwa, kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa.
katika nchi za Ufaransa na Uingereza ambako utaiti huo umeafanywa umebaini kuwa, nchini Ufaransa upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi umeanza kutokea tangu mwanzoni mwa 1990 ambapo hapo awali iliaminika kuwa, kupungua kwa uwezo wa mbegu za kiume kulitokana na sababu kama vile mtindo wa maisha, ulaji na matumizi ya dawa kupindukia na matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi, lakini safari hii utafiti umebaini kuwa matumizi ya nguo za ndani yamekuwa yakiwaathiri wanaume wengi.
Mtafiti wa Uingereza, Profesa Richard Sharpe kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema kuwa, tatizo hilo linaweza kuepukwa ikiwa mhusika atajitahidi kuvaa nguo zinazokubalika na mahala alipo. Hata hivyo, anapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.
Post A Comment: