ads

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema wala rushwa ni sawa na wauaji.


Akihubiri leo wakati wa sikukuu ya Pasaka kwenye Kanisa la Azania Front, Lwiza alisema rushwa ni adui wa haki na inaweza kusababisha hadi vifo.

Alisema licha ya rushwa kuwepo tangu enzi za kifo cha Yesu Kristolakini madhara yake yamekuwa makubwa katika jamii hadi sasa.

Alisema baada ya Yesu Kristo kufufuka katika kaburi, walinzi walipewa rushwa ili wasiseme ukweli kuwa amefufuka bali waseme amechukuliwa na wanafunzi wake.

“Kwa hiyo viongozi waliwapa rushwa walinzi ili wasiseme ukweli na hivyo wakatoa taarifa za uongo, rushwa inapofusha macho,” alisema. 

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: