.Arsenal imeanzisha mazungumzo na kocha wa Juventus, Max Allegri wakati hatima ya Arsene Wenger ikiwa njia panda.
Gazeti la SunSport imebainisha kuwa Gunners imekuwa na mawasiliano na Allegri katika siku saba zilizopita katika kuangalia uwezekano wa kumchukua Mtaliano huyo kushika mikoba ya Wenger.
Hivi karibuni kiongozi moja wa Arsenal alikuwa hafahamu kama Wenger ataendelea kubaki klabu hapo, wakato kocha huyo akiendelea kupata matokeo mabovu na kuongeza shindikizo kutoka kwa mashabiki.
Pia, kuna taarifa kuwa klabu hiyo inahitaji mkurungezi wa ufundi na winga wa zamani wa klabu hiyo Marc Overmars ametajwa kujaza nafasi hiyo.
Hata hivyo, Wenger anajua kuwa kuna mambo yanayoendelea nyuma yake.
Mwenendo wa kusuasua wa Arsenal kwa sasa umewalazimisha viongozi kufuatilia Allegri ( 49) mwenye mafanikio makubwa kwa sasa.
Mtaliano huyo ametwaa ubingwa wa Serie A na Kombe la Italia katika misimu yake miwili ya kwanza akiwa na Juventus na sasa pia yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa taji msimu huu.
Jumanne iliyopita aliingoza Juventus kuichakaza Barcelona kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Jambo zuri zaidi ni kwamba Allegri mwaka jana alimaliza masomo yake ya Kiingereza akiwa ni maandalizi ya kuachana na miamba ya Serie A na kutimikia Ligi Kuu England.
Kocha huyo pia alikuwa akitakiwa na Chelsea kuziba pengo la Jose Mourinho, lakini kwa bahati mbaya nafasi akiangukia kwa Antonio Conte.
Post A Comment: